Monday, April 4, 2016
Fastjet Shikamoo! Kwa kweli Tanzania hii inahitaji mabadiliko makubwa
sana kwenye sekta ya usafiri wa anga. Nadhani Fastjet bila kutazamwa na
serikali wamejiwekea uzio wa
kutokamatika kisheria. Jana usiku saa 3:15 tumeruka kutoka JNIA kuelekea
KIA na tulipokaribia kutua control tower wakaripoti kuwa kuna hitilafu
ya umeme hivyo hatuwezi kutua kwa sababu taa za runway zimezima.
Tukarudishwa NIA..tukaambiwa ndege inajaza mafuta turudi KIA kwa sababu
tatizo limekwisha. Wakati tunashangaashangaa tunashushwa kwenye ndege
na kuambiwa kuwa masaa ya crew yamekwisha hivyo tusingeweza kuruka tena.
Na wanasema ndege iliyopo ni ya leo saa 5 asubuhi. Wamekataa kutoa
nafasi kwa ndege ya saa 12 asubuhi KIA - Jomo Kenyatta ambayo inaweza
kubeba abiri wote tulioshindwa kutua KIA usiku wa jana. Maamuzi yote
yanafanywa London,...tumepiga simu London kwa simu zetu na kueleza ugumu
uliopo kwetu abiria na udhalili wa mazingira ya airport kama mnavyoona
kwenye picha akina mama wamelala kwenye conveyor belt baada ya uchovu
kuwazidia. Jitihada zetu zimeishaia patupu..na ukweli wenzetu wa ulaya
hawaoni kama sisi huku unyanini tunastahili kupata treatment kama watu
wa huko kwako. Tumepata emergency lakini wao wanaichukulia kama kitu ya
kawaida sana. Hapa kuna watoto wadogo..wagonjwa...wamama wajawazito...na
watu wenye mahitaji maalum. Fastjet kwa kujidai wao ni "low cost"
airline hawatoi malazi, nauli za kurudi majumbani, chakula wala
viburudisho panapotokea kuahirishwa kwa safari. Nimemua nikae hapa na
wenzangu kama 60 nione mwisho wake itakuwaje. Wanachokifanya Fastjet ni
kinyume na Conventions na Protocol zinazohusu usafiri wa anga pamoja na
sheria yetu ya ndani..masharti yao kwenye mtandao ambayo ni sehemu ya
ticket yanamkandamiza sana abiria bila kujali sheria za ndani na
kimataifa wa hali halisi kwa wakati husika..hiki kiburi wamekipata wapi?
Nataka nikirejea nipeleke petition ya kufanya yafuatayo: moja ni kupata
declaration kuwa Fastjet haistahili kuwa kwenye category ya "low cost
airlines " na pili ilazimishwe kutekeleza matakwa ya sheria za kitaifa
na kimataifa za uendeshaji wa huduma za usafiri wa anga na wawajibike
kisheria kwa mteja kwa wanavyofanya Precision Air na ATCL...nadhani
katika Afrika ni Tanzania peke yake ambapo Fastjet inaendeshwa kama
local flight na hizo local flights nasikia zina faida zaidi ya maradufu
kulinganishwa na international flights. Nchi yetu kwa nini tuteseke? Au
kuna watu wanafurahia hawa akina Fastjet kuendelea kuiibia ATCL soko la
ndani kwa hila na kuwahi ticket mapema kwa 200,000/= na kulipa 700,000/=
siku ya safari au kwa kubadili siku au muda wa kusafiri?. Sitasubiri
raisi awatumbue....watanikuta FCT...#pingaukoloni na unyonyaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment