Maelezo juu ya Sarafu mpya ya elfu 50,000 bofya hapa
JARIBU BAHATI YAKO KWA KUBOFYA HAPO JUU
BENKI
Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. Gavana wa BoT,
Profesa Benno Ndulu, amesema kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini
ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na
haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina
yoyote.
Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya
Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema
sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo
na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa Gavana Ndulu, kutolewa kwa sarafu hiyo
kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za
aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali
muhimu ya kitaifa na kimataifa.
“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi
huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa
Ndulu.
Gavana
Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000
katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo
kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu
yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi
kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji
zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya
hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa
Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’.
Upande
mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu
na miaka 1964-2014. JARIBU BAHATI YAKO KWA KUBFYA KWENYE MAELEKEZO
YALIYOPO HAPO CHINI
No comments:
Post a Comment