Maafisa nchini Indonesia wamesema hukumu ya kuwanyonga watu wanne kwa
kukutwa na hatia ya makosa ya dawa za kulevya imetekelezwa.
Mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo Noor Rachmad amesema raia
watatu wa Nigeria na Muindonesia mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi
katika gereza la kisiwa cha Nusa Kambangan.
Mapema wiki hii mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo amesema watu 14, wengi wao wakiwa ni wageni watanyongwa.
Serikali mbalimbali za kigeni, Makundi ya haki za binadamu na ndugu za
watu hao walizitaka Mamlaka nchini Indonesia kuacha kuwaua watu hao.
No comments:
Post a Comment